LAINI 12896 Zafungiwa Kwa Utapeli

Filed in Habari by on 17/01/2025 0 Comments
LAINI 12896 Zafungiwa Kwa Utapeli

LAINI 12896 Zafungiwa Kwa Utapeli

LAINI 12896 Zafungiwa Kwa Utapeli

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kuzifungia laini za simu 12,896 kutokana na kujihusisha na vitendo vya ulaghai wa mtandaoni kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Kwa mujibu wa ripoti ya TCRA ya robo ya pili ya mwaka wa fedha 2024/2025, matukio ya ulaghai kwa njia ya simu yamepungua kwa asilimia 19 kutoka 16,002 kati ya Julai na Septemba 2024 hadi 12,896 kati ya Oktoba na Desemba 2024.

Hii ni punguzo la laini 3,106 ndani ya kipindi hicho.

Aidha, ripoti hiyo imetaja mikoa inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya laini za simu, ambapo Dar es Salaam unaongoza kwa laini milioni 15.9. Mkoa wa Mwanza unafuata kwa kuwa na laini milioni 5.8, Arusha milioni 5.2, Mbeya milioni 4.9, na Dodoma ikiwa na laini milioni 4.2.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!