Kung’olewa Viti Benjamin Mkapa Simba iwajibike

Filed in Michezo by on 16/12/2024

Kung'olewa Viti Benjamin Mkapa Simba iwajibikeKung’olewa Viti Benjamin Mkapa Simba iwajibike

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imesikitishwa na vitendo vya mashabiki kung’oa na kuharibu viti vya kukalia watazamaji katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Simba Sport Club ya Tanzania na Club Sportif Sfaxien ya Tunisia uliofanyika jana tarehe 15 Desemba, 2024.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Prof. Palamagamba Kabudi amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuchukua hatua mara moja kwa kuwaandikia timu ya Simba Sports Club na kuwanakiri Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF) ili gharama za uharibifu uliosababishwa wakati mechi hiyo zilipwe.

Mheshimiwa Waziri Kabudi amewataka mashabiki wanaoingia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuacha vitendo vya uharibifu wa uwanja kwa kuwa wanasababisha hasara kwa Serikali na kuharibu ubora wa uwanja.

“Vitendo vilivyofanyika jana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa havikubariki na sio vya kimichezo, nakuelekeza Katibu Mkuu kuchukua hatua mara moja. Pamoja na kuwaandikia Simba Sports Club na TFF, wapeni ushirikiano Polisi ili watu wote waliokuwa wanang’oa viti na kuvitupa wakamatwe na wachukuliwe hatua za kisheria, lazima tabia hii ikomeshwe” amesema Prof. Kabudi.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limesema kuwa katika fujo hizo shabiki mmoja wa timu ya CS SFAXIEN aliumia na kupatiwa huduma ya kwanza na kuruhusiwa, huku viti vya rangi ya blue 156 na Orange 100 viling’olewa na mashabiki hao.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments are closed.

error: Content is protected !!