JINSI ya Kumchukulia Mtu Kitambulisho Cha NIDA

JINSI ya Kumchukulia Mtu Kitambulisho Cha NIDA
JINSI ya Kumchukulia Mtu Kitambulisho Cha NIDA
Kufuatia baadhi ya wananchi kutochukua Vitambulisho vyao vilivyokuwa katika ofisi za Kata, Vijiji, Mitaa na Shehia, Vitambulisho hivyo sasa vimekusanywa na kurudishwa katika ofisi za NIDA za Wilaya.
Ukipokea Ujumbe Mfupi wa simu (SMS) fika ofisi ya NIDA Wilaya uliko jisajili kuchukua Kitambulisho chako.
NIDA imesema kuwa mtu atakayeshindwa kuchukua Kitambulisho chake ndani ya mwezi mmoja toka kupokea ujumbe mfupi wa simu, matumizi ya Namba yake ya Utambulisho wa Taifa (NIN) yatasitishwa.
Aidha NIDA imesema kuwa Mwombaji yeyote aliyepata sms ya kuchukua Kitambulisho chake na angependa kuchukuliwa Kitambulisho chake na mtu mwingine, inaruhusiwa.
Anachotakiwa ni kufika katika ofisi ya NIDA ya Wilaya husika akiwa na sms iliyotumwa kwa mwenye Kitambulisho kwaajili ya uthibitisho.

JINSI ya Kumchukulia Mtu Kitambulisho Cha NIDA
