JINSI ya Kujaza Fomu ya Maombi ya Pasipoti Online
JINSI ya Kujaza Fomu ya Maombi ya Pasipoti Online
Hatua za Ujazaji Fomu Ya Maombi Ya Pasipoti Kwa Njia Ya Kielektroniki (Mtandao).
Muongozo wa Maombi ya Pasipoti
VIELELEZO VINAVYOHITAJIKA WAKATI WA UJAZAJI WA FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI
- Cheti cha Kuzaliwa Mwombaji
- Cheti/Kiapo cha Kuzaliwa Mzazi wa Mwombaji
- Kitambulisho cha Taifa
- Picha ya Mwombaji ya hivi karibuni yenye kivuli cha rangi ya buluu isiyokoza (Light blue Background)
- Ada ya Fomu Tsh 20,000
- Ushahidi wa Safari au Ushahidi wa Shughuli anayofanya Mwombaji.
JINSI YA KUJAZA FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI
- Bofya Anza kujaza fomu, kwa Ombi Jipya
- Bofya ENDELEA ili kuendelea na Ombi ambalo halikufikia mwisho
- Utahitajika Kujaza Namba ya Utambulisho (Rfeference ID) wa Ombi lako na Namba ya Ombi (Application Number) husika
- Jaza Taarifa zako sahihi kwa ukamilifu
- Hifadhi Namba yako ya Utambulisho (Application ID) kwa matumizi ya baadaye.
- Jaza Taarifa za Pasipoti ya zamani (ikiwa uliwahi kuwa na pasipoti)
- Jaza Taarifa za Wadhamini na Watu ambao ungependa wapewe taarifa endapo utatakewa na tatizo lolote
- Ambatanisha Vielelezo vyote vinavyohitajika (kwa kuzingatia maelekezo)
- Hakiki Taarifa zako zote na kisha bofya kukubaliana nazo ikiwa ziko sahihi
- Lipia fomu yako baada ya kupatiwa Namba ya Kumbukumbu ya Malipo (Control Number)
- Kitufe cha Kufuatilia Hali (Status) ya Ombi kinakuwezesha kufuatilia Ombi lako limefikia hatua gani.
OMBI JIPYA
Kwa Mwombaji anayeanza kujaza fomu ya maombi ya Pasipoti kwa njia ya kielektroniki kwa mara ya kwanza (hata kama alishawahi kuwa na pasipoti).
Wakati wa ujazaji wa fomu ya maombi ya pasipoti, Mwombaji anatakiwa kujaza taarifa zake kwa usahihi na ukamilifu, na mara atakapomilisha atapatiwa Namba ya Ombi (Application Number) na Namba ya Utambulisho (Reference ID) ya Ombi lake.
ENDELEZA OMBI
Kwa Mwombaji ambaye alishajaza fomu ya maombi ya pasipoti kwa njia ya kielktroniki na kufikia hatua ya kupatiwa Namba ya Ombi.
Hatua hii itampa fursa ya kurekebisha taarifa zake au Kupakua na kuichapisha fomu yake.
Ni hatua muhimu katika kuendeleza ombi la Mteja ambalo halikufikia hatua ya mwisho.
Ili kuweza kuendelea na Ombi lako ulilofanyia maombi ya kwenye mfumo huu wa mtandao, tafadhari weka namba ya Ombi yako sambamba na taarifa za msingi ulizojaza wakati unafanya ombi lako.
UFUATILIAJI WA OMBI
Kwa Mwombaji ambaye alishajaza fomu ya maombi ya pasipoti kwa njia ya kielktroniki na kufikia hatua ya kupatiwa Namba ya Ombi.
Hatua hii itampa fursa ya kurekebisha taarifa zake au Kupakua na kuichapisha fomu yake.
Ni hatua muhimu katika kuendeleza ombi la Mteja ambalo halikufikia hatua ya mwisho.
NB: Baada ya Mwombaji Kukamilisha Kujaza taarifa zake, atafahamishwa ya Kwamba usajili Umekamilika na Kupatiwa namba ya Ombi, ambayo ni Muhimu aiandike Pembeni na Kuihifadhi Kwa Kumbukumbu za Baadae.
Kisha atapewa namba ya Kumbukumbu ya Malipo (Control Number) na Kutakiwa Kwenda Kulipia Malipo ya awali (Advance Fee) ya Tsh 20,000.
Baada ya Kukamilisha Usajili, na Kupatiwa namba ya Ombi na namba ya Kumbukumbu (Control Number)
Utaratibu wa Malipo ya ada ya huduma ya Pasipoti Kwa Kutumia M-pesa/Tigopesa
- Ingia Kwenye Menu Ya M-pesa/tigopesa (*150*00#/*150*01#)
- Bonyeza Namba 4 (Lipa Kwa M-pesa) – Voda Bonyeza Namba 4 (Kulipia Bili) – TIGO
- Kisha Weka/Ingiza Namba ya Kampuni
- Ingiza Namba (888999)
- Ingiza kumbukumbu Namba(Ingiza Control Number inayoanzia na 99109…….)
- Ingiza kiasi (kama ulivyo elekezwa Mfano: 20,000 nk.)
- Utapata Maelezo kuwa unalipa pesa NMB
- Ingiza Namba ya Siri kuhakiki
Utapata Meseji toka M-Pesa/ Tigopesa kama muamala umekubalika; - Utapata meseji kutoka kwenye mfumo Namba 15200 kama muamala umekubalika;
- Mteja atatakiwa kurudi katika Ombi Linaloendelea:
- Kisha ataingiza namba Ya Ombi/Simu na namba ya risiti
- Na hapo ataweza kupakua Fomu yake ya Maombi
- Ataiwasilisha Fomu hiyo katika Ofisi ya Uhamiaji Makao makuu au Afisi Kuu Zanzibar
Utaratibu wa Malipo ya ada ya huduma ya Pasipoti Kwa Kutumia Benki za NMB na CRDB
- Jaza fomu ya malipo ya kielectroniki;
- Fuata maelekezo kama yanavyojieleza kwenye fomu;
- Utapata meseji toka benki;
- Utapata meseji toka kwenye mfumo Namba 15200 kama muamala umekubalika.
