JINSI ya Kufanya Usajili wa Vizazi na Vifo Kidijitali

Filed in Makala by on 01/12/2024

JINSI ya Kufanya Usajili wa Vizazi na Vifo KidijitaliJINSI ya Kufanya Usajili wa Vizazi na Vifo Kidijitali

Kupitia Makala hii utaweza kufahamu namna ya kupata cheti cha kuzaliwa pamoja na kifo katika maeneo yako wakati wowote ule.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Hauhitaji kwenda Wilayani mpaka pale utakapoambiwa cheti chako cha kuzaliwa au kifo kipo tayari.

Nini unatakiwa Kufanya?
Hakikisha una nyaraka halisi (original) zinazothibitisha taarifa zako ambazo ni pamoja na:

  • Tangazo la Kizazi.
  • Kadi ya Kliniki.
  • Cheti cha Ubatizo.
  • Pasi ya Kusafilia.
  • Cheti cha Kumaliza Shule ya Msingi au Sekondari (Living Cerificate).
  • Kitambulisho cha Mpiga kura au kitambulisho cha utaifa cha Mwombaji.
  • Vitambulisho vya mpiga kura au vya taifa vya wazazi.
  • Picha ya mwombaji ya hivi karibuni yenye kivuli cha rangi ya buluu isiyokoza (Light Blue Background).

Kwa ambaye hana cheti cha kumaliza sekondari (Living Certificate) au bado hajamaliza shule anatakiwa kuwa na barua ya Utambulisho toka kwa Mkuu wa Shule au Mwalimu Mkuu wa Shule husika.

Mfano wa barua hizo unapatikana katika Stationery iliyo karibu na wewe kwa msaada zaidi.

Zingatia/Muhimu
Mwombaji lazima aambatanishe vielelezo si chini ya viwili kati ya hivyo vilivyotajwa pamoja na vitambulisho vya mpiga kura au taifa vya wazazi.

Wapi unapaswa Kwenda Kufanya Maombi ya Cheti Cha Kuzaliwa?

Tembelea Stationery Mbalimbali zinazotoa huduma za internet zilizopo karibu nawe kwaajili ya kufanya maombi hayo.

Kwanini Usajili wa Vizazi na Vifo kwa Njia ya Mtandao?

  • Inamsaidia mteja kufanya maombi ya cheti cha kuzaliwa au kifo mahali popote alipo yaani kwenye kata yake anayoishi bila kuhitaji kufika katika Ofisi za Wilaya.
  • Mteja anaweza kufuatilia maendeleo ya maombi yake akiwa nyumbani na sio kwenda Wilayani.
  • Cheti kinatolewa ndani ya siku tano (5) za kazi tangu kupokelewa kwa maombi husika.
  • Mteja anayo nafasi ya kufanya maombi muda wowote na siku yeyote hata siku za jumamosi, jumapili na sikukuu ambazo kimsingi si siku za kazi.
  • Mteja ataweza kupewa majibu ya maombi yake ikiwa ni pamoja na maelekezo ya kufanya pale ambapo kuna mapungufu katika maombi yake bila kuhitaji kufika katika Ofisi za Wilaya.
  • Mteja atatakiwa kufika Ofisi ya RITA Wilayani pale tu atakapoambiwa cheti chake kipo tayari na anaweza kufika Ofisini kukichukua na si vinginevyo.
  • Huduma hii inamwondolea mteja/mwananchi usumbufu wa kusafili mara kwa mara kwenda Wilayani kufuatilia cheti chake kama kimeishatoka.
  • Cheti kinatolewa kwa wakati na hivyo kumwezesha mteja kukidhi mahitaji yake kama kupeleka mtoto shule, kuomba kazi, kufanya maombi ya bodi ya mikopo ya Elimu ya juu nakadharika.
  • Huduma hii inamsaidia mteja kuendelea na majukumu yake mengine.
  • Huduma ya usajili wa Vizazi na Vifo kwa njia ya mtandao ni rahisi na haraka sana.

KAURI MBIU: FANYA USAJILI WA VIZAZI NA VIFO KWA NJIA YA MTANDAO UPATE CHETI CHAKO NDANI YA SIKU TANO ZA KAZI. WATOTO, WAZAZI, WALEZI TUWAJIBIKE


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments are closed.

error: Content is protected !!