JINSI ya Kuangalia Matokeo ya Kidato Cha Pili FTNA 2024
JINSI ya Kuangalia Matokeo ya Kidato Cha Pili FTNA 2024
Ili kuangalia matokeo ya mtihani wa kidato cha Pili (FTNA) mwaka 2024, wanafunzi na wazazi wanaweza kuangalia Matokeo ya Kidato cha Pili Kwa kutembelea tovuti rasmi ya NECTA au kutumia huduma za simu za mkononi.
Kwa urahisi na uhakika zaidi, unashauriwa kutumia tovuti rasmi ya NECTA.
Njia hii inawawezesha kupata matokeo sahihi na ya papo kwa papo, popote pale ulipo.
Nijuze Habari tumekuwekea hatua kwa hatua namna na jinsi ya kuangalia matokeo ya mtihani wa kidato cha Pili mwaka 2024 hapa chini.
Ili uweze kuangalia Matokeo ya Kidato cha Pili 2024.
Tembelea Tovuti ya NECTA
Kwa kuanzia, fungua kivinjari chako cha wavuti kama kwenye Chrome, Firefox, au Safari.
- Kisha, andika anwani ya tovuti ya NECTA www.necta.go.tz.
- Nenda Kwenye Sehemu ya Matokeo (Results)
- Bonyeza sehemu iliyoandikwa “Results” au “Matokeo.” itakupeleka kwenye ukurasa unaoonesha orodha ya matokeo ya mitihani mbalimbali inayosimamiwa na NECTA.
- Baada ya kufungua sehemu ya matokeo, utaona orodha ya mitihani kama vile PSLE, CSEE, na SFNA wewe Chagua Mtihani wa FTNA.
- Chagua Mwaka wa Mtihani, kwa kuwa unatafuta matokeo ya mwaka 2024, chagua mwaka 2024 kwani pia matokeo ya miaka iliyopita yameorodheshwa hapo.
- Baada ya kuchagua mwaka, utaona orodha ya shule zote zilizofanya mitihani wa kidato cha Pili mwaka 2024.
- Tafuta jina la Shule ambayo Mtoto wako alisomea/ulisomea na bonyeza jina la shule hiyo Majina ya Wanafunzi yote na matokeo yao yataonekana.
Kwa urahisi unaweza kutazama Matokeo ya Form Two Kwa kubofya MATOKEO YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2024.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: JINSI ya Kuangalia Matokeo ya Kidato Cha Pili FTNA 2024