JEZI Mpya za Yanga CAF Champions League 2024/2025
JEZI Mpya za Yanga CAF Champions League 2024/2025
Klabu ya Young Africans, leo Jumatano Novemba 20,2024 imezindua jezi mpya ambazo itazitumia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League 2024/2025).
Yanga imetinga hatua ya makundi ya michuano hiyo na mechi yake ya kwanza itapigwa Novemba 26, 20204 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar Es Salaam.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo, Ally Kamwe amesema kuwa kuwa Jezi hizo zitauzwa kwa shilingi elfu 50 na zitauzwa Kwa bei rejareja tu, hakutakuwa na bei ya jumla.
Aidha Jezi hizo zitauzwa Makao Makuu ya Klabu hiyo Jangwani na katika maduka yote ya GSM Malls.
