JEZI Mpya za Simba CAF Confederation Cup 2024/2025

Filed in Michezo by on 20/11/2024 1 Comment

JEZI Mpya za Simba CAF Confederation Cup 2024/2025JEZI Mpya za Simba CAF Confederation Cup 2024/2025

Klabu ya Simba leo Novemba 20,2024 imezindua jezi mpya ambazo itazitumia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Simba SC imetinga hatua ya makundi ya michuano hiyo na mechi yake ya kwanza itapigwa Novemba 27,2024 kwenye Uwanja Benjamin Mkapa, Jijini Dar Es Salaam.

Jezi zilizozinduliwa ni za aina tatu za nyumbani, ugenini na jezi mbadala (third kit) na zimetengenezwa na Mzalishaji wao wa siku zote Sandaland The Only One.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa Jezi hizo zitakuwa zinapatikana kwenye maduka ya Sandaland The Only One.

Ahmed Ally ameongeza kuwa Kwenye jezi hizo (Mo Cola) ndio mdhamini Mkuu na atakaa hapo hadi fainali.”

JEZI Mpya za Simba CAF Confederation Cup 2024/2025

JEZI Mpya za Simba CAF Confederation Cup 2024/2025

Jezi zitauzwa kwa Tsh. 45,000 kwenye maduka ya Sandaland na zimekuja kwa idadi maalumu hivyo kama unahitaji jitahidi uwahi kununua.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Murtaza Mangungu amesema kuwa jezi ni nzuri na naamini Wanasimba watajitokeza kununua kwa wingi.

“Kipekee tunamshukuru Sandaland kwa utekelezaji wa haya mambo, jezi ni nzuri na naamini Wanasimba watajitokeza kununua kwa wingi. Tunawashukuru Mo Cola kwa udhamini na tunaamini fedha watakazotoa zitatusaidia katika michuano hii.”

“Tumekubaliana na MOI kwamba tutafanya zoezi la uchangiaji wa damu na hii itakuwa sehemu ya kutoa kwa jamii. Nawaomba Wanasimba kujitokeza kuchangia damu. Hakuna sehemu duniani damu inauzwa, ni jambo muhimu sana kujitoa kwa wenye uhitaji wa damu.”- Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu.

Kwa upande wa Mtengenezaji Sandaland amesema kuwa aliwaahidi Wanasimba kutawaletea jezi nzuri na amemefanya kama alivyoahidi, huku akitaka wanasimba kuendelea kuiunga mkono timu yao.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments (1)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Edson James says:

    Hakika sandaland ni unyama mwingi kama vpi ubaya ubwelaa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!