HISTORIA ya DK Emmanuel Nchimbi Mgombea Mwenza wa Urais CCM 2025

HISTORIA ya DK Emmanuel Nchimbi Mgombea Mwenza wa Urais CCM 2025
HISTORIA ya DK Emmanuel Nchimbi Mgombea Mwenza wa Urais CCM 2025
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye leo amepitishwa kuwa Mgombea Urais (CCM) kwenye Uchaguzi wa mwaka huu 2025, amemtangaza Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea mwenza wake wa Urais.
Akiongea leo January 19,2025 kwenye Mkutano Mkuu Maalum Jijini Dodoma, Rais Samia amesema Dkt. Nchimbi ataendelea kuwa Katibu Mkuu wa CCM kwa sasa hadi Uchaguzi Mkuu utakapofanyika.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefikia hatua hiyo baada ya Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kumwandikia barua ya kuomba apumzike Umakamu wa Rais ambapo amesema baada ya kutafakari ameridhia ombi hilo lakini kwa sasa Dkt. Mpango ataendelea kuwa Makamu wa Rais hadi utakapofanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025.
Hii hapa Historia ya DK Emmanuel Nchimbi Mgombea Mwenza wa Urais Kupitia CCM – 2025.
Dk Emmanuel Nchimbi alizaliwa Desemba 24, 1971, mkoani Mbeya, atafikisha miaka 54 December mwaka huu 2025.
Elimu yake ya msingi aliipata jijini Dar es Salaam, katika Shule ya Msingi Oysterbay kati ya mwaka 1980 na 1986.
Baba yake, Mzee John Nchimbi, ni askari mstaafu wa Jeshi la Polisi na alihitimu utumishi wake akiwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara.
Mzee Nchimbi pia aliwahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kupitia kundi la majeshi, na baadae Katibu wa CCM wa Mkoa.
Hata hivyo, aliachana na siasa ulipoanzishwa mfumo wa vyama vingi.
Dk Nchimbi aliendelea na elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Uru (1987-1989) kwa kidato cha kwanza hadi cha tatu.
Kisha akahamia Shule ya Sekondari Sangu, ambako alihitimu kidato cha nne (1989-1990).
Kidato cha tano na sita alisoma katika Shule ya Sekondari Forest Hill, Mbeya, kati ya mwaka 1991 na 1993.
Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, alijiunga na kilichokuwa Chuo cha IDM Mzumbe, Morogoro, ambapo alihitimu Stashahada ya Juu ya Utawala (1994-1997).
Dk Nchimbi amemuoа Jane Nchimbi na wamejaaliwa watoto watatu.
Dk Nchimbi alianza safari ya kisiasa akiwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) mwaka 1997 na baadaye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mwaka 1998.
Mwaka 2003, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda.
Mwaka 2005, alianza harakati za ubunge Jimbo la Songea Mjini, akashinda uchaguzi huo kwa asilimia 67.6 na kutetetea tena kiti chake tena mwaka 2010 kwa ushindi wa asilimia 59.9.
Akiwa mbunge, alihudumu kama Naibu Waziri katika wizara mbalimbali, ikiwemo Habari, Utamaduni na Michezo (2006), Kazi, Ajira na Vijana (2006-2008), na Ulinzi na Kujenga Taifa (2008-2010).
Mwaka 2010, alipanda na kuwa Waziri kamili, akihudumu katika Wizara ya Habari na baadae Wizara ya Mambo ya Ndani hadi December 2013.
December 3, 2016, Dk Nchimbi aliteuliwa na Rais wa awamu ya tano, hayati John Magufuli, kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazili.
Baadae, Rais Samia Suluhu Hassan alimhamishia kuhudumu kama Balozi wa Tanzania nchini Misri.
January 15, 2024, Dk Nchimbi aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM katika kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichofanyika Zanzibar, kuchukua nafasi ya Daniel Chongolo aliyejiuzulu November 29, 2023.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: HISTORIA ya DK Emmanuel Nchimbi Mgombea Mwenza wa Urais CCM 2025