HESLB Waliopata Mkopo Awamu ya Tatu 2024/2025

Filed in Education by on 20/10/2024 0 Comments

HESLB Waliopata Mkopo Awamu ya Tatu 2024/2025

WANAFUNZI 19,345 WAPANGIWA MIKOPO YA TZS 59.49 BILIONI AWAMU YA TATU 2024/2025

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya JUU (HESLB) Leo Jumapili, Oktoba 20, 2024) imetangaza Awamu ya Tatu (Batch Three) yenye wanafunzi 19,345 wa shahada ya awali waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 59.49 bilioni kwa mwaka wa masomo 2024/2025.

Wanafunzi hawa 19,345 ni wapya wa mwaka wa kwanza wanaojiunga na taasisi mbalimbali za Elimu ya juu zilizopo nchini kwaajili ya masomo ya shahada za awali (Bachelor Degrees).

Idadi ya wanafunzi wa shahada ya awali waliopangiwa yafikia 70,990

Kufuatia kutangazwa kwa Awamu ya Tatu, jumla ya wanafunzi wapya wa shahada za awali waliopangiwa mikopo imefikia 70,990 na thamani ya mikopo yao ni TZS 223.3 bilioni, wanafunzi wa kiume ni 40,164 (56.58%) na wa kike ni 30,825 (43.42%).

Mikopo kwa Stashahada

Aidha, katika awamu hii pia, wamo wanafunzi wapya wa stashahada 425 (wa mwaka wa kwanza 378 na wanaoendelea na masomo 47) ambao wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 1.1 bilioni.

Ruzuku ya ‘Samia Scholarship

Mpaka sasa, jumla ya kiasi cha TZS 3.02 bilioni kimetolewa kwa ajili ya ruzuku kwa wanafunzi 599; (588 awamu ya kwanza na 11 awamu ya pili) wa mwaka wa kwanza wanaonufaika na ‘Samia Scholarship’ kwa mwaka wa masomo 2024/2025.

KUANGALIA KAMA UMEPATA MKOPO BOFYA HAPA


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!