HESBL Wanafunzi 11,256 Wapangiwa Mikopo kwa Rufaa 2024/2025

Filed in Education by on 03/12/2024

HESBL Wanafunzi 11,256 Wapangiwa Mikopo kwa Rufaa 2024/2025HESBL Wanafunzi 11,256 Wapangiwa Mikopo kwa Rufaa 2024/2025

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESBL) imetangaza Wanafunzi 11,256 Waliopangiwa Mikopo ya Tzs 36.4 Bilioni kwa Rufaa.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Idadi ya Wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopata mkopo kwa njia ya rufaa ni 4,183 yenye thamani ya TZS 13.8 bilioni.

Idadi ya Wanafunzi wa mwaka wa pili na kuendelea waliopata mkopo kwa njia ya rufaa ni 7,073 yenye thamani ya TZS 22.5 bilioni.

Mpaka sasa jumla ya mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza imefikia 79,573 yenye thamani ya TZS 250.9 bilioni.

Upangaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2024/2025 umefika kikomo, waombaji ambao hawajafanikiwa kupata wanashauriwa kuomba mkopo awamu ijayo dirisha litakapofunguliwa.

Mkurugenzi Mtendaji,
Imetolewa na: Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Dar es salaam, Jumatatu, Disemba 02, 2024.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags: ,

Comments are closed.

error: Content is protected !!