FOMU za Kujiunga na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)
FOMU za Kujiunga na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)
VETA imeweka utaratibu maalum kwaajili ya kujiunga ili kupata mafunzo katika vyuo inavyovimiliki. Utaratibu ni kama unavyoelezwa hapa chini:
Kwa mafunzo ya muda mrefu, yyuo vyote hutangaza nafasi za kujiunga mwezi wa Agosti kila mwaka. Matangazo hutolewa katika vyombo vya habari nchini pamoja na kwenye tovuti ya www.veta.go.tz
Mwombaji ni lazima awe amemaliza elimu ya msingi, sekondari na kuendelea.
Mwombaji ni lazima awe amemaliza elimu ya msingi, sekondari na kuendelea.
Mwombaji huchukua fomu katika chuo chochote kilichopo karibu. Fomu hizo zina taarifa ya vyuo vyote vinavyomilikiwa na VETA, ikiwa ni pamoja na fani zinazofundishwa na mahali chuo kilipo na kama ni kutwa au bweni.
Mwombaji anaruhusiwa kufanya mtihani wa kujiunga mkoa aliochukua fomu lakini anaweza kuchagua kusoma mkoa wowote anaochagua kulingana na mahitaji yake.
Mwombaji anatakiwa kufanya mtihani wa kujiunga (Aptitude Tests) mwezi Oktoba na wale wanaofanikiwa kuchaguliwa hupewa taarifa mwezi Decemba ili kuanza masomo Januari mwaka unaofuata.
Mwombaji anayefanikiwa hupewa barua ya kujiunga inayofafanua mahitaji yote muhimu. Mahitaji yanatofautiana toka chuo kimoja hadi kingine na kutegemeana na fani aliyoomba, na pia kama ni kutwa au bweni.
Kwa utaratibu huu Mwombaji anaanza kujiunga na daraja la 1(Level 1) ambalo ni daraja la chini. Waombaji wanaoendelea madaraja ya juu (Level II-III) vigezo ni ufaulu wa daraja husika unamwezesha kupanda daraja lingine.
- ARUSHA VTC
- KAGERA VTC
- KARATU DVTC
- CHATO DVTC
- DAR ES SALAAM RVTSC
- KARATU DVTC
- KIHONDA RVTSC
- MABALANGA VTC
- MARA VTC
- MTWARA RVTSC
- PWANI RVTSC
- SIMANJIRO DVTC
- TABORA RVTSC
- URAMBO DVTC
- DAKAWA VTC
- IRINGA RVTSC
- KANADI VTC
- KILINDI DVTC
- KITANGALI DVTC
- LINDI RVTSC
- MAKETE DVTC
- MIKUMI VTC
- MOSHI RVTSC
- MWANZA RVTSC
- NGORONGORO DVTC
- NYASA DVTC
- RUANGWA DVTC
- SINGIDA VTC
- TANGA RVTSC
- DODOMA RVTSC
- IRINGA DVTC
- KAGERA RVTSC
- KIPAWA ICT CENTRE
- KONGWA DVTC
- MANYARA RVTSC
- MKINGA DVTC
- MPANDA VTC
- NKASI DVTC
- SHINYANGA VTC
- SONGEA VTC
- ULYANKULU VTC

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: FOMU za Kujiunga na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)