FOMU ya Rufaa Matokeo ya NECTA
FOMU ya Rufaa Matokeo ya NECTA
MAELEKEZO MUHIMU
- Hakikisha unajaza taarifa sahihi katika fomu hii. Unapaswa kuandika anwani yako
kamili ambayo itatumika katika mawasiliano ya kukupatia matokeo ya usahihishaji upya wa skripti yako/zako. - Gharama ya kusahihishiwa upya ni shilingi 20,000/= kwa somo moja.
- Malipo kwaajili ya kusahihishiwa rufaa yafanyike kwa kutumia namba maalum (Control Number)
inayotolewa na mfumo wa malipo ya serikali kwa kieletroniki (GePG) kupitia tovuti ya NECTA: www.necta.go.tz. - Malipo yote yafanyike kupitia benki za NMB, CRDB na NBC au kwa kutumia mitandao ya kifedha ya T-Pesa (TTCL), M-Pesa (Vodacom), Tigo Pesa (Yas), Ezy Pesa (Zantel), na Airtel Money (Airtel)
- Endapo utajaza taarifa zisizo sahihi ambazo zitasababisha kusahihisha skripti nyingine tofauti na matarajio yako, fedha uliyolipa HAITARUDISHWA na itakupasa kulipa tena gharama za usahihishaji wa rufaa yako.
- Unapaswa kurudisha fomu ya rufaa (RF2) pamoja na risiti ya malipo kwa Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani Tanzania, S.L.P 2624 Dar es Salaam, kabla ya kipindi
cha rufaa kumalizika (ndani ya mwezi mmoja tangu tarehe matokeo yalipotangazwa). - Unatakiwa kutoa nakala ya fomu (RF2) na risiti ya malipo na kubaki navyo kama kumbukumbu yako.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD FOMU YA RUFAA
