FOMU ya Maombi ya Hati ya Kusafiri ya Dharura Online
FOMU ya Maombi ya Hati ya Kusafiri ya Dharura Online
Hii ni huduma mpya inayomuwezesha muombaji kujaza Fomu ya Maombi ya Hati ya Dharura kwa njia ya Kielektroniki kutokea popote alipo, Baada ya kujaza fomu hiyo mtandaoni na kuambatanisha picha yake kama atakavyoelekezwa mtandaoni, atatakiwa kuichapisha (Print) fomu hiyo na kufika nayo katika Ofisi ya Uhamiaji iliyo karibu naye kwa ajili ya kushughulikiwa maombi yake ya Hati ya Dharura.
Huduma hii itamwondolea usumbufu wa kwenda ofisini kuchukua fomu ya maombi ya pasipoti, na badala yake ataipata na kuijaza fomu hiyo mtandaoni.
Aidha, huduma hii itasiaidia katika kuimarisha utunzaji wa kumbukumbu na baadae kumwezesha mteja kufuatilia hatua lilipofikia ombi lake kwa njia ya mtandao.
Ili kuweza kufanya maombi ya Hati ya Dharura, Mwombaji anatakiwa kuwa na vielelezo vifuatavyo:-
- Cheti Chake cha Kuzaliwa;
- Cheti/Kiapo cha Kuzaliwa mmoja wa wazazi wake;
- Picha ya (Passport Size) yenye rangi ya bluu bahari nyuma;
- Vielelezo vya Ushahidi wa Safari;
Barua ya maombi ya Hati ya Dharura (ielekezwe kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, S.L.P 512, Dar Es Salaam);
NB: Viambato vyote ni lazima viwe kwenye mfumo wa PDF na kila Kiambato kisizidi ukubwa wa Kb 1032.
Picha (Passport size) ya Muombaji yenye rangi bluu bahari nyuma, iwe kwenye mfumo wa JPG, PNG au JPEG.
Unasisitizwa Kunakiri Namba yako ya ombi pindi atumapo ombi kwa ajili ya kumbukumbu
Fomu ichapwe katika fomati ya A4
BOFYA HAPA KWA MUOMBAJI ANAYEENDELEA
