FAHAMU Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo
FAHAMU Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuwafahamisha wananchi kuwa vitambulisho vya Taifa vimechapishwa na kusambazwa maeneo mbalimbali.
Kadhalika, orodha ya majina ya watu wote ambao vitambulisho vyao vimechapishwa imewekwa kwenye tovuti ya Mamlaka kupitia kiunganishi https://vitambulisho.nida.go.tz
Hivyo, mwananchi ambaye hujachukua kitambulisho chako, unaweza kufahamu kwa kupitia tovuti hii Ofisi ya serikali ya Mtaa/Kijiji ambapo kitambulisho chako kipo kwa ajili ya kukichukua.
Aidha, unaweza kutembelea tovuti ya Mamlaka kupitia www.nida.go.tz kisha bofya mahali palipoandikwa Kitambulisho cha Taifa ikifuatiwa na Fahamu Kitambulisho kilipo.
Baada ya hapo ukurasa unaoonyesha mikoa utafunguka, Chagua mkoa na kufuatiwa na wilaya uliyojisajili na baadae bonyeza Kata ikifuatiwa na Kijiji/Mtaa uliokuwa unaishi wakati unajisajili.
Baada ya hapo ukurasa wenye orodha ya majina na mahali Kitambulisho chako kilipo utafunguka.
Ukiona jina lako tafadhali nenda kachukue Kitambulisho chako mahali kilipo mapema kwani baada ya mwezi mmoja kupita vitarejeshwa ofisi za NIDA za wilaya.
Hivyo utalazimika kukifuata katika ofisi ya NIDA ya Wilaya uliyojisajili.
NIDA Orodha ya Majina ambao Vitambulisho vyao vipo tayari Kila Mkoa.
CHAGUA MKOA WA MAHALI ULIPO JIANDIKISHA
NIDA VITAMBULISHO KWA NGAZI YA MIKOA
kupata namba ya kitambulisho cha nida bofya hapa, Jinsi ya kupata kitambulisho cha nida kupitia simu yako, Jinsi Ya Kupata Namba Ya NIDA (NIN) Online Bure, Tembelea website ya NIDA kujua kama kitambulisho chako kipo tayari.
FAHAMU UMUHIMU WA KUWA NA KITAMBULISHO CHA TAIFA
Ewe Mwananchi, sasa unaweza kutumia Namba yako ya Utambulisho wa Taifa (NIN)/Kitambulisho cha Taifa (NID) kupata huduma nyingi za kijamii, kiuchumi na kiusalama :-
- Kusajili Laini ya Simu (Sim Card Registration),
- Kusajili Namba Maalumu ya Mlipa Kodi (TIN),
- Kusajili Biashara/Kampuni – BRELA,
- Kukata Hati ya Kusafiria ya Kielektroniki (E-Passport),
- Kukata Leseni ya Udereva,
- Kupata Huduma ya Afya,
- Kufungua Akaunti ya Benki,
- Kukopesheka Kirahisi kwenye Taasisi za Fedha,
- Kujiunga na Elimu Ngazi Mbalimbali,
- Kupata Mkopo wa Elimu ya Juu,
- Hati Miliki ya Kiwanja, Nyumba n.k,
- Kujidhamini na Kudhamini Wengine,
- Kitambulisho cha Taifa kutokana na kuwa na Kisilikoni (Cheap) kinaweza Kutumika kama Pochi ya Fedha ya Kielektroniki (E-Wallet) ambako unahifadhi fedha na kufanya malipo kwa kutumia Kitambulisho Chako,
- Kitambulisho kinaweza kutumika kama ATM CARD,
- Kwenye Maingio ya Malango Kielektroniki (E-Entrace),
- Daftari la Mahudhurio la Kielektroniki (Electronic Attendance),
- Mwananchi kuondokana na Adha ya Kubeba Utitiri wa Vitambulisho kwani sasa taarifa zote Muhimu za mwananchi zitapatikana katika Mfumo Mkuu wa Taifa wa Utambuzi wa Watu,
- Kinaweza kutumika kama hati ya Utambuzi wa Utaifa wa wananchi wanaovuka mipaka ndani ya nchi zilizoko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwingineko.
- Vitaimarisha Utendaji Kazi Serikalini kwa Kuwa na Kumbukumbu Sahihi za Watumishi na Malipo ya Stahili zao, hasa Wanapostahafu,
- Kupata Ruzuku za Pembejeo za Kilimo Kirahisi,
- Kujisajili kwenye Chama cha Ushirika (Wakulima, Wavuvi, Wafugaji na Makundi mengine),
- Kupata Msaada wa TASAF unaotolewa kwa Kaya Masikini,
- Kufungua Akaunti za Benki,
- Kuomba Ajira pamoja na Huduma Nyingine Nyingi.
