ELIE Mpanzu Kuitumikia Simba lini?
ELIE Mpanzu Kuitumikia Simba lini?
Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Simba SC, Elie Mpanzu ataanza kuitumikia Klabu hiyo katika Michuano ya Kombe la Shirikisho la CAF (CAF Confederation Cup 2024/2025) January 2025.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ametoa ufafanuzi kuwa dirisha dogo la usajili la CAF litafunguliwa Januari 01 na kufungwa Januari 31 2025 wakati dirisha dogo la TFF likifunguliwa Disemba 16 na kufungwa Januari 15 2025.
Hivyo Mpanzu ataanza kuitumikia Simba Ligi Kuu ya NBC kuanzia wiki ijayo baada dirisha la TFF kufunguliwa lakini atalazimika kusubiri Januari 1 ili asajiliwe katika kikosi cha Simba kinachoshiriki kombe la Shirikisho.
“Disemba 15 litafunguliwa dirisha dogo la usajili wa ndani na Ellie Mpanzu atasajiliwa hapo kwa maana hiyo mechi yoyote ya ndani baada ya tarehe 15 atakuwa sehemu ya kikosi lakini dirisha la CAF ni mpaka Januari, 2025 kwahiyo mechi yoyote ya kimataifa kuanzia January atakuwa sehemu ya kikosi,” alisema Ahmed
