CAF Yataja Faini atakayekiuka Kanuni
CAF Yataja Faini atakayekiuka Kanuni
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza adhabu kwa timu zote zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho zitakazoshindwa kuzingatia kikamilifu maagizo yake.
Klabu ya Young Africans na Simba SC ni miongoni mwa klabu zitakazoshiriki katika Michuano hiyo hatua ya Makundi.
Kwa mujibu wa Kanuni, adhabu hizo ni kama ifuatavyo;
- Kutumia mpira usio rasmi wakati wa mechi faini yake ni hadi dola za Kimarekani 40,000 kutoka 30,000.
- Kutumia nembo isiyo rasmi faini yake ni hadi dola 10,000 kutoka 2,000.
- Kutoheshimu rangi za vifaa vinavyowasilishwa na CAF faini yake ni hadi dola 40,000 kutoka 10,000.
- Kutoonekana kwa majina ya wachezaji kwenye jezi faini yake ni hadi dola 20,000 kutoka 5,000.
- Benchi la ufundi ambalo litatumia mavazi yenye chapa ambayo haijaidhinishwa faini yake ni hadi dola 60,000.
