CAF yaisogeza mbele michuano ya CHAN 2024

CAF yaisogeza mbele michuano ya CHAN 2024
CAF yaisogeza mbele michuano ya CHAN 2024
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limetangaza kuahirisha michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) yatakayofanyika nchini Kenya, Tanzania, na Uganda hadi mwezi wa Agosti 2025.
Wataalamu wa ufundi na miundombinu wa CAF, ambao baadhi yao wako nchini Kenya, Tanzania na Uganda, wameomba muda wa ziada ili kuhakikisha kwamba miundombinu na vifaa viko katika kiwango kinachohitajika ili kuandaa michuano hiyo ya Afrika.
Hata hivyo taasisi hiyo inaonyesha kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda kwa ujenzi na uboreshaji wa viwanja vya michezo, viwanja vya mazoezi, hoteli, hospitali na miundombinu na vifaa vingine kwaajili ya kufanikisha maandalizi ya michuano ya Mataifa ya Afrika.
Mashindano hayo yalipangwa kufanyika kuanzia Februari 1 hadi Februari 28, 2025 kulingana na ratiba ya kwanza, sasa yatafanyika mwezi August 2025.
Rais wa CAF Patrice Motsepe amesema kuwa “Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Rais William Ruto wa Kenya, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa uongozi wao, kujitolea na hatua kubwa iliyofikiwa katika ujenzi na uboreshaji wa viwanja, viwanja vya mazoezi, hoteli, hospitali na miundombinu na vifaa vingine katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda ili kufanikisha michuano ya Mataifa ya Afrika. Nimefurahishwa na ujenzi na ukarabati unaoendelea wa miundombinu na vifaa vya soka nchini Kenya, Tanzania na Uganda. Nina imani kwamba viwanja vya mazoezi, hoteli, hospitali na miundombinu na vifaa vingine vitafikia viwango vinavyohitajika na CAF kuandaa michuano ya Mataifa ya Afrika yenye mafanikio makubwa mwezi Agosti 2025″.
Aidha Droo ya michuano hiyo itaendelea kawaida Jumatano ya January ari 15, 2025 jijini Nairobi.
Tarehe kamili ya kuanza kwa Michuano ya Mataifa ya Afrika itatangazwa na CAF hapo baadae.

CAF yaisogeza mbele michuano ya CHAN 2024
