BODI ya Ligi yatoa tamko Yanga kuhamia KMC Complex
BODI ya Ligi yatoa tamko Yanga kuhamia KMC Complex
BODI ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara (TPLB) imethibitisha kupokea barua ya klabu ya Young Africans ya kuomba kuutumia uwanja wa KMC Complex kwa michezo yake ya nyumbani badala ya Azam Complex ambako walikuwa wanautumia awali ingawa ombi hilo bado halijatolewa majibu.
Akizungumzia ombi hilo, Afisa Habari wa TPLB, Karim Boimanda amesema kuwa Ombi la Yanga Sc linaangukia kwenye kanuni ya tisa ya TPLB inayotoa ruhusa kwa klabu ambayo haina uwanja wa nyumbani kuchagua uwanja mwingine ambao utakuwa ndani ya mkoa ule ule ambao walikuwa wanacheza ama mkoa wa jirani ilimradi uwe unakidhi vigezo.
“Barua ambayo Young Africans Sc wameiandikia Bodi ya Ligi inaeleza kuwa klabu hiyo haina uwanja, wameshamalizana na wamiliki wa uwanja wa Azam Complex, Chamazi kwa hiyo wanakwenda kuangukia kwenye hiyo kanuni ya 9 ibara ya 4.” amemaliza Boimanda.
