Bi. Zubeda Hassan Sakuru Mrithi wa CEO Francois Regis
Bi. Zubeda Hassan Sakuru Mrithi wa CEO Francois Regis
Uongozi wa Simba umetangaza kusitisha mkataba na aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo, Francois Regis raia wa Rwanda.

CEO Francois Regis atupigwa Virago Simba SC
Taarifa ya Simba iliyotolewa November 23, 2024, imesema kuwa: “Tunapenda kuutarifu umma kuwa Klabu ya Simba imefikia makubalino ya kusitisha mkataba na ndugu Francois Regis ambaye alikuwa ni Mtendaji Mkuu kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Tunamshukuru Mr. Regis kwa kipindi alichohudumu katika klabu yetu.
“Bodi imefanya uteuzi wa Bi. Zubeda Hassan Sakuru kama Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu.

Bi. Zubeda Hassan Sakuru CEO Mpya Simba SC
“Bi.Zubeda yuko mbioni kuhitimu Shahada yake ya kwanza ya Uzamivu, ana Shahada mbili za Uzamili katika Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Warwick, Uingereza na Chuo Kikuu cha Mzumbe Tanzania. Pia ana Shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe.
“Bi.Zubeda amefanya kazi kama Meneja Miradi wa Simba akimsaidia Bw. Kajula kuhusu mchakato wa kutengeneza sera na ushauri wa masuala ya kiutendaji.”
Aidha Zubeda alikuwa mbunge wa viti maalum kupitia Chadema mwaka 2015 hadi 2020.
Regis anaondoka Simba baada ya kukaa takribani miezi minne pekee tangu atambulishwe klabuni hapo Julai 26, 2024 akichukua nafasi ya Imani Kajula.

Bi. Zubeda Hassan Sakuru CEO Mpya Simba SC
