BEI Mpya za Mafuta ya Petroli December 2024

Filed in Habari by on 05/12/2024

BEI Mpya za Mafuta ya Petroli December 2024BEI Mpya za Mafuta ya Petroli December 2024

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano ya tarehe 4 Desemba 2024 saa 6:01 usiku.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Kwa mwezi Desemba 2024, bei za rejareja na za jumla katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ni kama
zinavyoonekana katika Jedwali Na. 1 na 2, mtawalia.

Jedwali 1: Bei Kikomo za Rejareja (Shilingi/Lita)Bei za mafuta za rejareja kwa maeneo mbalimbali ya miji, wilaya na mikoa ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 3.

Bidhaa za mafuta zinazoagizwa na kupokelewa hapa nchini zinazingatia bei za mafuta yaliyosafishwa (FOB) kutoka soko la Uarabuni. Mwezi Desemba 2024, bei kikomo za mafuta zimekokotolewa kwa kuzingatia bei za soko la Uarabuni za mwezi Novemba 2024.

Ikilinganishwa na Mwezi Oktoba 2024, bei za mwezi Novemba zimepungua kwa
asilimia 0.29 kwa mafuta ya petroli; kuongezeka kwa asilimia 2.11 kwa mafuta ya dizeli na asilimia 2.28 kwa mafuta ya taa.

Gharama za uagizaji mafuta (Premiums) zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 7.26 kwa petroli na kupungua kwa asilimia 12.80 kwa dizeli na wastani wa asilimia 7.10 kwa mafuta ya taa katika Bandari ya Dar es Salaam; hakuna mabadiliko katika Bandari ya Tanga; na zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 15.67 kwa mafuta ya petroli na
hakuna mabadiliko kwa mafuta ya dizeli katika Bandari ya Mtwara.

Gharama za mafuta (FOB) na gharama za uagizaji (Premiums) zinalipiwa kwa kutumia fedha za kigeni ikiwemo Dola ya Marekani. Kwa bei za mwezi Desemba 2024, wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni (Applicable Exchange Rate) umepungua kwa 2.72.

Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 3. Aidha, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 2.

Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka AGIZO hili.

EWURA inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla na rejareja pamoja na jamii kuzingatia yafuatayo: –

Bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo.

Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei
za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA
itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.

Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya
ushindani isipokuwa bei hizo zisizidi bei kikomo (Price cap) au kuwa chini
ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama zilivyokokotolewa kwa mujibu wa
Kanuni za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2022 zilizotangazwa tarehe 28 Januari 2022 kupitia Gazeti la Serikali Na. 57 na marekebisho ya Kanuni tajwa kupitia Gazeti la Serikali Na. 761A la tarehe 30 Oktoba 2023 na Mabadiliko ya Kanuni za Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja za Mwaka 2024.

Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei za mafuta, punguzo, vivutio vya kibiashara vinavyotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana
kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo
vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa
kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja.

Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.

Wauzaji wa bidhaa za mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa stakabadhi za mauzo
kutoka kwenye Electronic Fiscal Pump Printers (EFPP) na wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo,
tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita.

Stakabadhi hizo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora unaotakiwa.

Stakabadhi hizo pia zitasaidia
kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya bidhaa za mafuta ya petroli.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments are closed.

error: Content is protected !!