AbduHamid Moalin Mkurugenzi wa Ufundi Young Africans

Filed in Michezo by on 18/11/2024 0 Comments

AbduHamid Moalin Mkurugenzi wa Ufundi Young AfricansAbduHamid Moalin Mkurugenzi Mpya wa Ufundi Young Africans

Klabu ya Young Africans Leo November 18, 2024 imemtangaza AbduHamid Moallin kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Klabu hiyo.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mara ya mwisho nafasi hiyo kuwepo Yanga ilikuwa mwaka 2016, Mkurungenzi akiwa Hans van Pluijm baada ya usajili wa George Lwandamina.

Kabla ya kujiunga na Young Africans, AbduHamid Moallin alikuwa Kocha Mkuu wa KMC FC ya Kinondoni Jijini Dar Es Salaam.

Kutokana na Kutangazwa Kwa Moallin, Kuanzia sasa ndiye Msimamizi Mkuu wa Dira na Masuala yote ya Kiufundi ndani ya Young Africans.

Kwa lugha ya kawaida huyu ndiye Kiunganishi kati ya Uongozi na benchi la ufundi la Young Africans.

Baada ya Uteuzi huo Moallin amesema kuwa ana furaha kuwa sehemu ya klabu hiyo, kuwa sehemu ya historia yake, na kuwa sehemu ya mafanikio ya siku zijazo.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!