7 Wafariki Ajali ya Magari Matatu Karagwe

Filed in Habari by on 04/12/2024

7 Wafariki Ajali ya Magari Matatu Karagwe7 Wafariki Ajali ya Magari Matatu Karagwe

Watu saba wamefariki Dunia na wengine 9 kujeruhiwa katika Ajali ya Magari Matatu iliyotokea eneo la Kihanga Wilayani Karagwe mkoani Kagera.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Ajali hiyo ilihusisha lori la mizigo aina ya scania lenye namba za usajili T 621 EGQ, ambalo liliigonga Haice yenye namba T 367 DJD inayofanya safari zake kati ya Karagwe na Mutukula.

7 Wafariki Ajali ya Magari Matatu Karagwe

7 Wafariki Ajali ya Magari Matatu Karagwe

Sambamba na Costa yenye namba za Usajili T 367 ESP, inayofanya safari zake kati ya Bukoba na Karagwe mkoani Kagera jana tarehe 3 Desemba 3,2024.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema chanzo ni uzembe wa dereva wa Scania.

Amesema, dereva huyo alikuja akiwa na mwendo mkali akayagonga magari hayo mawili yaliyokuwa na abiria ambayo yalisimama yakiwa yanakaguliwa na maafisa kutoka Idara ya Uhamiaji kwenye eneo la ukaguzi

7 Wafariki Ajali ya Magari Matatu Karagwe

7 Wafariki Ajali ya Magari Matatu Karagwe

“Katika vifo hivyo saba kuna wanawake wanne, mwanaume mmoja na watoto wawili, kwenye majeruhi kuna wanaume wanne na wanawake watano.

“Chanzo ni uzembe wa dereva, kama ingekuwa mfumo wa breki umefeli asingeumaliza mteremeko na kona zilizo karibu na eneo la ajali, pia kuna vibao vinaonesha simama ukaguliwe.

“Ni wazi baada ya kumaliza mteremko hakuchukua tahadhari za barabarani, chanzo ni uzembe tu kutochukua tahadhari.”

7 Wafariki Ajali ya Magari Matatu Karagwe

7 Wafariki Ajali ya Magari Matatu Karagwe

Aidha, Kamanda huyo ametoa rai kwa madereva kutambua hizo barabara sio zao pekee kwani wanatumia na watumiaji wengine.

“Kulikuwa na haja gani ya dereva kuja na spidi aliyokuja nayo? Ukiangalia madhara ya Hiace aliyoigonga ni ishara alikuwa spidi kali sana.

“Nasikia ametoroka haitomsaidia, ajisalimishe mwenyewe kabla hatujampata, tuna mkono mrefu hawezi kutukimbia akasalimika,”amesisitiza Kamanda Chatanda.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments are closed.

error: Content is protected !!