421 Waitwa Kwenye Usaili Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA)
MAJINA 421 ya Walioitwa Kwenye Usaili Kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Kuitwa Kwenye Usaili NECTA, Walioitwa kwenye Usaili Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
- Usaili wa kuandika na vitendo utafanyika tarehe 17 Oktoba, 2024 katika Kituo cha Baraza la Mitihani la Tanzania (Mbezi Wani) kilichopo Mbezi Makonde, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Kila msailiwa atapaswa kufika eneo la usaili saa 1:00 asubuhi.
- Usaili wa mahojiano ya ana kwa ana kwa watakaofaulu usaili wa kuandika na vitendo utafanyika tarehe 18 Oktoba, 2024 katika Ofisi za Baraza la Mitihani la Tanzania Mikocheni, Eneo la Viwanda, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Kila msailiwa atapaswa kufika eneo la usaili saa 1:00 asubuhi.
- Msailiwa anapaswa kuwa na Kitambulisho cha Kazi kwaajili ya utambuzi.
- Msailiwa ambaye hatakuwa na kitambulisho hataruhusiwa kufanya usaili.
- Msailiwa anatakiwa kufika na Vyeti Halisi ambavyo ni cheti cha kuzaliwa, Kidato cha IV, Kidato cha VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada, Usajili wa Bodi za Kitaaluma, Leseni na vinginevyo kutegemeana na sifa za Mwombaji.
- Msailiwa ambaye hatakuwa na vyeti halisi hataruhusiwa kufanya usaili.
- Msailiwa atawajibika kujigharamia chakula, usafiri, malazi au gharama zozote zitakazojitokeza.
- Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE au NECTA).