MAJINA 393 ya Walioitwa Kwenye Usaili Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) anapenda kuwaarifu waombaji wa nafasi za kazi za muda kupitia programu maalum ya kuendeleza zao la Pamba nchini zilizotangazwa tarehe 18.09.2024 nafasi imetolewa kwaajili ya usaili kwa waombaji ambao hawakuweza kuhudhuria usaili wa awamu ya Kwanza na ya Pili.
Awamu ya Tatu ya usaili imepangwa kufanyika tarehe 11.10.2024 katika Kampasi ya Edward Moringe Mjini Morogoro.
Aidha, waombaji watakaofaulu katika mchakato huo watapangiwa vituo vya kazi.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili huo ni wale tu waliokidhi vigezo kutokana na sifa zilizoainishwa katika tangazo la kazi na wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo: –
- Usaili wa awamu ya Tatuw a kuandika utafanyika tarehe 11.10.2024 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo.
- Kila Msailiwa anapaswa kufika na moja kati ya vitambulisho vifuatavyo: -Kitambulisho cha Mkazi, kazi, Mpiga kura, Uraia au Hati ya Kusafiria.
- Kila Msailiwa anapaswa kufika na VYETI HALISI,vya kuzaliwa, Sekondari (kidato cha IV, VI), Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada kutegemeasifa za Mwombaji.ila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
- Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali pakufanyia usaili.
- Msailiwa haruhusiwi kuingiana simu au kifaa chochote cha kielekroniki kwenye chumba cha usaili.
Waombaji ambao majina yao hayataonekana kwenye usaili wa awamu ya kwanza, pili na tatu watambue kuwa hawakukidhi vigezo vilivyoainishwa katika tangazo la kazi.
MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA
Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi
zitakapotangazwa kwakuzingatia vigezo vya tangazo husika.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Post Views: 121