1399 WAITWA KWENYE USAILI MWANGA DISTRICT COUNCIL

Filed in Usaili by on 27/09/2024 0 Comments

1399 WAITWA KWENYE USAILI MWANGA DISTRICT COUNCIL

MAJINA 1399 YA WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA MWANGA 26-09-2024

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kwa cheo cha Mwandishi Mwendesha ofisi Daraja la II, Mtendaji wa Kijiji Daraja la III na Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 03/10/2024 hadi 08/10/2024 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

  • Usaili utafanyika kwa kuzingatia tarehe za usaili kama zilivyoainishwa kwa kila kada kwenye jedwali hapo chini. Muda wa kuanza usaili utakuwa saa moja kamili asubuhi (1:00 asubuhi) na sehemu ambapo usaili utafanyikia itakuwa kama jedwali linavyonesha kwa kila kada.
  • Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi; 
  • Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, leseni ya udereva, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Barua ya Utambulisho kutoka ofisi za serikali ya kijiji/mtaa au Hati ya kusafiria.
  • Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Astashahada(Certificate), Stashahada(Diploma) na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji na viambatisho alivyoweka wakati anatuma maombi.
  • Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
  • Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
  • Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
  • Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
  • Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
  • Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.
  • Hali ya hewa ya Wilaya ya Mwanga inabadilikabadilika hivyo ikiwa mwili wako haustahimili hali ya baridi/upepo unashauriwa kuja na nguo ya kuzuia baridi.

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!