1,230,780 KUFANYA MITIHANI YA KUHITIMU ELIMU YA MSINGI 2024
Wanafunzi 1,230,780 wamesajiliwa na wanatarajiwa kufanya mitihani ya kuhitimu Elimu ya Msingi kuanza leo 11 hadi kesho September 12, 2024, kati yao Wavulana ni asilimia 46 na Wasichana ni asilimia 54.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA), Dkt. Said Mohamed amesema kuwa masomo yatakayotahiniwa ni sita ambayo ni Kiswahili, English, Sayansi na Teknolojia, Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi na Uraia na Maadili.
Baraza la Mtihani Tanzania(NECTA) limewatahadharisha kuwafutia matokeo wanafunzi watakaobanika kufanya udanganyifu.
Dkt. Said Mohamed, amesema kuwa watahiniwa wenye mahitaji maalumu waliosailiwa kufanya mtihani huo ni 4,583 kati yao 98 ni wasioona,1402 wenye uoni hafifu,1067 wenye uziwi, 486 wenye ulemavu wa akili na 1530 ni wenye ulemavu wa viungo.
“Kati ya watahiniwa 1,230,780 waliosajiliwa kufanya mtihani mwaka 2024, watahiniwa 1,158,862 sawa na asilimia 94.16 watafanya mtihani wa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 71,918 sawa na asilimia 5.84 watafanya mtihani wa lugha ya kiingereza ambayo wamekuwa wakiitumia katika kujifunzia,”amesema katibu huyo.
Nijuze Habari inawatakia kila la kheri watahiniwa wote katika mitihani hiyo ya kumaliza Elimu ya Msingi mwaka huu 2024.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Post Views: 78